Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, amesema kuwa atakabidhi majina ya familia 12 kwa Makamu wa Rais Dkt Mpango zinazomiliki Ranchi ya Usangu ambayo imekuwa ikitumiwa tofauti na malengo.
Balile ameyasema hayo katika kongamano la Wahariri na Wadau wa Uhifadhi wa Mazingira, na utunzaji wa vyanzo vya maji, linalofanyika Mkoani Iringa hii leo Decemba 19, 2022 lililohudhuriwa na wadau mbalimbali.
”Ranchi ya Usangu ukiuliza wanakwambia hawajui nani anayeimiliki lakini sisi tunafanya habari za uchunguzi inamilikiwa na familia 12 na hizi familia wamo majaji wamo wabunge wamo mawaziri haya tunayoyasema majina tunayo na tutakukabidhi na tunajua kwamba wasaidizi wako haya hawawezi kusema” amesema Balile.
”Lakini kwa masikitiko makubwa zaidi hii lunch ilikuwa iimeondolewa na govement notes namba 28 kwenye hili eneo maana ni shingo inayotumia kuingiza mifugo kwenye bonde la Ihefu ila makubaliano ya mawaziri wanane Makamu wa Rais amerejesha hii Ranchi ambayo kila ukiuliza wanakuambia hatujui ni nani anaimiliki”
”Orodha inafahamika ipo viongozi wa ulinzi na usalama wanayo sasa tulisema kama hawatakukabidhi Mhe. Makamu wa Rais mimi naomba kujitolea nitakukabidhi. Askari wa Ruaha wanapambana na majangili wanaovuna samaki kwa kuchota na chepe na kutumia bodaboda kusafirisha ambapo bodaboda hizo zinalipwa laki tatu kwa siku na bodaboda hizo zinamilikiwa na baadhi ya Viongozi” amesema Balile.
”Majangili wa samaki wanachimba na kutoa samaki kwa chepe, sasa bodaboda mmoja akisafirisha samaki analipwa laki tatu kwa siku kwahiyo kuna bodaboda nyingi sana zinaingia lakini ukiangalia wakubwa ambao wananunua hizi bodaboda ni wanasiasa ni miradi yao wanavuna samaki hizi familia 12 zinatutesa sisi tunaendelea kuteseka”