Takriban watu 78 wamefariki dunia, katika kipindi cha zaidi ya wiki moja wakati wa majira ya baridi nchini Afghanistan, jambo ambalo limezidisha mgogoro wa kibinadamu nchini humo.
Kwa mujibu wa Msemaji wa Wizara ya usimamizi wa majanga Taliban, Shafiullah Rahimi amesema vifo hivyo vimetokea tangu Januari 10, 2023.
Rahimi ameongeza kuwa, zaidi ya mifugo 75,000 pia wamefariki kutokana na baridi kali na kwamba athari inaweza kuwa kubwa kutokana na takwimu zinazoendelea kutolewa.
Utawala wa Taliban, umekuwa ukijaribu kuwasaidia zaidi ya watu milioni moja kote nchini humo na bado wanajaribu kuzifikia familia nyingi zaidi.