Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amesema hakuna ushahidi wa moja kwa moja kwa Taifa la Urusi kuhusika na ajali ya helikopta iliyotokea jana katika jiji la Kyiv, na kuuwa watu 18 akiwemo Waziri wa Mambo ya Ndani na naibu wake.

Zelensky, ameyasema hayo wakati akizungumza kwa njia ya video kwenye Kongamano la Kiuchumi la Dunia, linalofanyika mjini Davos nchini Uswisi.

Amesema, licha ya kwamba hakuna anayehusika na tukio hilo ila kitendo kilichofanywa kwenye taifa lake ni matokeo ya vita inayoendelea nchini kwake.

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky

Aidha Zelensky ameongeza kuwa, “Wakati ambao ulimwengu huru hutumia kufikiria unatumiwa na serikali ya kigaidi kuua,” alielezea. Matamshi hayo yametafsiriwa kama ombi kwa Ujerumani kuharakisha kuwasilisha mizinga yake ya Leopard inayotamaniwa na Ukraine.”

Imeripotiwa kuwa Ujerumani haiko tayari kupeleka magari ya silaha isipokuwa Marekani itajitolea kutoa mizinga yake ya kivita ya Abrams ambapo wiki iliyopita Uingereza iliahidi kutuma mizinga yake kadhaa huko Kyiv.

Awali, Mkuu wa muungano wa kijeshi wa Nato alisema huko Davos jana (Januari 18, 2023), kwamba Ukraine inaweza kupokea msaada, usaidizi wa hali ya juu, silaha nzito na silaha za kisasa zaidi.

Pep Guardiola awakosoa mashabiki Man City
Serikali yatoa kipaumbele kugharamia miradi ya maji