Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amemtetea mshambuliaji wake Erling Braut Haaland kutokana na kutofunga kwenye michezo ya karibuni akisema kuwa wengi wanasahau haraka ubora waliokuwa nao.

Haaland alisajiliwa Manchester City mwanzoni mwa msimu huu akitokea Borussia Dortmund, kwa ada ya uhamisho wa Pauni Milioni 51.2.

Kocha Guardiola amesema: “Sisi tuna mchezo wetu, na tuna misingi yetu ya kucheza lakini jinsi tulivyocheza michezo miwili iliyopita haijamsaidia Haaland kufunga. Ni kosa langu mimi, sikuwaelewesha namna ya kushambulia”

Kuhusu ubora wa timu yake, Pep amesema: “Watu hawakumbuki kuhusu rekodi yetu, namna gani tulikuwa bora. Nikifa watu watazungumza jinsi Pep alivyokuwa bora, huo ndiyo ukweli”

Hadi sasa Haaland ameshaifungia Manchester City mabao 21 katika michezo 18 ya Ligi Kuu ya England aliyocheza hadi sasa.

Makamu wa Rais akemea wizi, uchepushaji wa maji
Zelensky aikingia kifua Urusi ajali ya chopa