Mashirika ya kutetea haki za wanawake na wafanyabiashara ya kuuza miili yao nchini Afrika ya Kusini, wameandamana hadi nje ya Mahakama ya Johannesburg baada ya mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 21 kushitakiwa akidaiwa kuhusika na tukio la vifo vya wadada sita wanaoaminika kuwa ni wafanyabiashara wenzao.

Mwanaume huyo, alikamatwa wiki iliyopita wakati Polisi walipogundua miili ya wasichana hao sita kwenye karakana ya kutengeneza magari katikati mwa jiji la Johannesburg, wakati wakichunguza kutoweka kwa mfanyabiashara mmoja wa ngono ambaye inadaiwa alionekana mara ya mwisho akiwa na mshukiwa.

Kwa mujibu wa Polisi, baadhi ya miili hiyo ilikutwa ikiwa imefungwa mikono na ni dhahiri walikuwa wamekaa kwenye jengo hilo kwa muda mrefu, huku Mwanamume huyo akitarajiwa kushiriki katika safu ya utambulisho siku ya Ijumaa (Oktoba 21, 2022), baada ya safu ya awali kutofanyika kutokana na Afisa wa Polisi aliyepewa jukumu la kuiendesha safu hiyo kutokuwepo.

Kundi la wafanyabiashara hao wa kuuza miili, walihudhuria kesi hiyo Mahakamani na kumkejeli mwanamume huyo wakati akiingia kizimbani wakitaka kitambaa kilichoficha uso wake kuondolewa huku baadhi yao wakificha utambulisho wa sura zao kwani wanatarajiwa kuwa mashahidi katika kesi hiyo.

Kwa mujibu wa msemaji wa Mamlaka ya Kitaifa ya Mashtaka, Phindi Mjonondwane, amesema familia za wahasiriwa bado hazijafahamishwa kwa kuwa vipimo vya DNA vinaendelea kufanywa na kusema, “Kwa hatua hii hatuna mtu yeyote kati ya waliofariki ambao wametambuliwa vyema, mchakato huo bado unaendelea.”

Hata hivyo, Waandamanaji wengine walitoa ujumbe katika mabango yenye kauli mbiu zinazotaka kukomeshwa kwa biashara ya ngono na ulinzi wa wafanyabiashara ya ngono, huku mwakilishi wa mtandao unaojishughulisha na masuala ya wanawake Wakfu wa Sisterhood, Nozipho Dlamini, akisema maeneo ambayo wafanyabiashara ya ngono wanafanya kazi yanapaswa kuwa salama.

Majaliwa awataka watumishi kutimiza matarajio ya Rais Samia
Waitaka Serikali iwape majibu matukio watu kutoweka