Viongozi wa Umoja wa Ulaya (EU), wanakutana hii leo Oktoba 19, 2022 kwenye hatua muhimu ya kujadili na kuhakikisha bei za juu za nishati pamoja na ukosefu wa bidhaa hazitosababisha matatizo zaidi kwenye mataifa yao yanayokabiliwa na changamoto na kuchochea vurugu.

Hatua hiyo, inakuja ikiwa tayari Wabunge AU wamekutana (Oktoba 18, 2022), kujadiliana mgawanyiko kati ya wanaotaka kuweka hatua ya kudhibiti bei ya gesi ili kushusha bei na wale wanaodhani hatua hiyo itachangia kukosekana wasambazaji na kuviuwa viwanda na biashara.

Kuhusu juhudi za Umoja wa Ulaya za kuwasaidia wananchi wake kukabiliana na ugumu wa maisha, mbunge wa kambi ya wasoshalisti na wademokrats wa bunge la Umoja wa Ulaya, Pedro Marques amesema “”Kujaribu kuzuia wimbi la wenye siasa za kizalendo ni suala linalohusu kuzisaidia familia zinazoteseka.”

Ameongeza kuwa, “Wafanyabiashara wadogo, hawawezi kubeba mzigo wa bei za nishati zinazoongezeka na tunao watu nchini Ufaransa wanaosema wameshachoka hawawezi tena kuvumilia sasa tunahitaji sera ya Ulaya kuhakikisha hakuna atakayeachwa nyuma.”

Waziri aishauri Serikali kufuta uhusiano na Iran
SONAMCU yaongeza hamasa vyama vya msingi