Mapigano ya zaidi ya wiki moja ya makundi ya waasi katika eneo la Kaskazini mwa Syria, linalodhibitiwa na Uturuki yamesababisha vifo vya watu 58 vya wapiganaji huku raia wengi wakiyakimbia makazi yao kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza.

Kwa mujibu wa shirika linalofuatilia masuala ya vita vya Syria, limesema mapigano hayo, yametoa fursa kwa wapiganaji wanaofungamana na mtandao wa kigaidi wa Al-Qaeda, kupata nguvu na ari ya mapambano.

Moja ya athari za mapigano ya zaidi ya wiki moja ya makundi ya waasi katika eneo la Kaskazini mwa Syria. Picha: TRT World.

Inaarifiwa kuwa, mapigano hayo yaliyoanza tangu Oktoba 8, 2022 ni miongoni mwa matukio yaliyosababisha umwagaji mkubwa wa damu katika kipindi cha miaka kadhaa ambapo waasi 48 na raia 10 wameuawa.

Nalo, shirika linalofuatia haki za binadamu la Syria lenye makao yake mjini London limesema mapigano makali yamekuwa yakishuhudiwa katika eneo tete la karibu na mpaka wa Uturuki na kwamba Uturuki imepeleka wanajeshi wake ukanda wa Azaz kuweka usalama kati ya pande zinazopigana.

Sababu madhara ya afya kwa Wanawake na Watoto zatajwa
Wakulima walipwe kwa wakati: Majaliwa