Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametaka kuimarishwa kwa usimamizi wa malipo ya wakulima wa Tumbaku na yalipwe kwa wakati ikiwemo kutafuta masoko ya uuzaji wa zao la Tumbaku na kutatua changamoto zilizopo ili waweze kuzalisha zaidi na kujiongezea kipato na kuinua uchumi wa nchi.

Majaliwa, ameyasema hayo wakati akizungumza na wadau wa zao la tumbaku wilayani Namtumbo kwenye ukumbi wa shule ya sekondari ya Nasuli, Ruvuma yaliyowajumuisha wakulima, wanunuzi, wenye viwanda, maafisa kilimo, wasambazaji mbolea na wenye mabenki.

Aidha, katika kufanikisha jambo hilo, Waziri Mkuu amewataka Warajis Wasaidizi wa Mikoa wakutane na viongozi wa vyama vikuu mara kwa mara kupata taarifa ya mwenendo wa vyama vyao huku akiwataka wakulima kuhamasishwa kuwa na umoja na kuimarisha vyama vyao badala ya kuanzisha vyama vingine kwenye maeneo ambayo hayana uhitaji wa kufanya hivyo.

Katika hatua ntyingine, Waziri Mkuu pia amewataka viongozi wa Chama Kikuu kufuatilia kwa karibu mwenendo wa vyama vya ushirika na kuchukua hatua stahiki kwa wakati na kusema, “Vyama Vikuu visimamie kikamilifu vyama vya msingi ili vyama hivyo viweze kutoa huduma stahiki kwa wanachama wao.”

Mzozo wasababisha mapigano, 58 wafariki
Waziri aishauri Serikali kufuta uhusiano na Iran