Watu wengi wenye akili ndogo, watakuwa wanajiuliza liko wapi tumbo la mama Afrika, tumbo la mama mzaa chema, tumbo lilowahi kuzaa kizazi cha “dhahabu” ( gold generation) cha viongozi shupavu, weledi, wenye vision walioitetemesha dunia.

Hata sasa msomaji wa Dar24 Media nawe huenda unajiuliza, Liko wapi tumbo lilomzaa Nyerere na Nkrumah? tumbo lilowatoa Nelson Mandela na Samora Machel? tumbo lilowaleta duniani Keneth Kaunda na Sekou Toure!.

Hao hawatoshi, lipo pia tumbo lilowazaa Ben Bella na Abdu Nasser! tumbo lilowalea Kenyata na Augustino Neto! Je? li wapi tumbo la mama Afrika lilomzaa Thomas Sankara na Amilcal Cabral! lilowazaa Sedar Senghor na Patrice Lumumba?

Sasa nadhani sote tunajiuliza, je? Kizazi cha mama Afrika kimefunga kuzaa watu wema? kimelaaniwa hadi kizae majahili, madikteta na ving’ ang’anizi wa madaraka? majizi ya mali za umma! wapenda kiki na umaarufu wa kulazimisha?

Lakini bila shaka Tumbo hilihili ninalolifahamu ndilo limezaa majambazi? madikteta ? Waasi, Wapenda madaraka, ving’ang’aniz, wauaji, wezi na hatma ya yote huenda linafuata swali jingine, Je? Ni nini kimelisibu tumbo la mama Afrika?

Usikose majibu ya maswali haya hivi karibuni kupitia hapa hapa Dar24 Media kujua uhalisia wa lilipo Tumbo la MAMA mzaa kizazi cha Dhahabu barani Africa.

Kocha Minziro anavyowindwa Ligi Kuu 2023/24
Julai 21 siku maalum ya Lionel Messi Marekani