Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro amefanya mabadiliko madogo kwa makamishna na makamanda wa Polisi watatu kwa lengo la kuongeza ufanisi kwenye mikakati ya kubaini, kuzuia na kukabiliana na uhalifu.
Katika taarifa iliyotolewa na msemaji wa jeshi la Polisi David Misime imeeleza Kamishna msaidizi wa polisi (ACP) Joseph Konyo amehamishwa kutoka kitengo cha maadili makao makuu ya polisi Dodoma na kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma.
Kamanda Konyo anachukua nafasi ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma (ACP) Simon Maigwa ambaye anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro.
Aidha taarifa inaeleza kuwa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro (ACP) Amon Kakwale amehamishwa katika kamisheni ya operesheni na mafunzo makao makuu ya polisi Dodoma.