Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Selemani Jafo amewaagiza wamiliki wa kumbi za starehe na burudani kuhakikisha sauti zitokanazo na shughuli zao hazizidi viwango vinavyokubalika kwa mujibu wa sheria.

Amesema hayo leo Jijini Dodoma wakati wa kutoa Tamko kwa umma juu ya udhibiti wa uchafuzi wa mazingira utokanao na kelele na mitetemo na kuwaagiza wamiliki wa maeneo ya burudani na starehe kuzingatia matumizi ya vipima kelele na vizuia sauti kama ilivyoelekezwa kwenye masharti yote ya leseni zao.

Aidha Waziri Jafo ametoa rai kwa viongozi wa Dini kupitia Kamati za Amani, kulijadili suala hili la Kelele na Mitetemo iliyopitiliza kutoka kwa baadhi ya nyumba za ibada ili kupata namna bora ya kuendesha ibada kwa maslahi mapana ya afya ya jamii.

Aidha, Waziri huyo ameutaka umma wa Watanzania kuhakikisha agenda ya kelele na mitetemo inakuwepo kwenye mikutano ya wakazi na kuwaomba wananchi kutoa taarifa kuhusu kero na mitetemo kwa Ofisi za Serikali za Mitaa au NEMC kwa Namba za bure

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Juni 30, 2021
Makamanda watatu wapanguliwa na IGP Sirro