Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba amethibitisha kupokea taarifa toka Serikali ya Israel kuhusu kifo cha Mwanafunzi Joshua Mollel aliyekuwa anasoma nchini Israel ambaye alitekwa nyara Oktoba 7, 2023 wakati kundi la Hamas liliposhambulia Israel.
Waziri Makamba amesema ameongea na baba ya marehemu Joshua Mzee Mollel kuhusu ujumbe huo, ambapo ujumbe huo umesema Mollel aliuawa mara tu baada ya kutekwa na kundi la Hamas.
Kwa sasa Serikali inaendelea na mpango wa awali wa kuwapeleka mzee Mollel na mwanafamilia mwingine pamoja na Afisa wa Serikali nchini Israel, kuungana na Balozi wetu na maafisa waliopo huko, kukutana na kuzungumza na mamlaka za nchi hiyo ili kupata taarifa za ziada. Kwa ridhaa ya familia, na itakapobidi, tutatoa taarifa za ziada.
Josua alikuwa miongoni mwa vijana 260 waliokwenda Israel kushiriki mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa vitendo chini ya mpango wa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Israel.
Yeye pamoja na mwanafunzi mwenzake Clemece Mtenga walitekwa na kuuawa na kundi la hilo mara baada ya kuanzisha mshambulizi dhidi ya Israel ambayo Mtenga alikwa Novemba 28, mwaka huu katika kijiji cha Kirwa,wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro.