Makamu wa Rais wa Bunge la Ulaya, Eva Kaili, ameshtakiwa kwa makosa ya ufisadi na kuwekwa kizuizini baada ya wachunguzi wa ubelgiji kukukuta mabegi yaliyojaa fedha nyumbani kwake kiasi cha dola 630,000 na kukamata pia kompyuta kadhaa na simu za mkononi.

Kaili, ambaye amekuwa akiunga mkono mabadiliko ya sera za wafanyakazi nchini Qatar, ni miongoni mwa washukiwa wannne waliokamatwa na kuzuiliwa na polisi dhidi ya makosa hayo ya ufisadi ambapo washukiwa wengine wawili wamechiwa huru huku wachunguzi wakipekuwa moja ya nyumba ya mbunge mwengine wa bunge la Ulaya.

Polisi imesema bado inaendelea na uchunguzi wa tuhuma za Kaili ambaye pia ni mbunge wa ulaya kutoka chama cha kisoshalisti cha Ugiriki, aliyepokea rushwa kutoka kwa watu wanaofanya kazi kwa niaba ya Qatar mwenyeji wa mashindano ya kombe la dunia, ili kushawishi mjadala wa kisera katika Umoja wa Ulaya.

Makamu wa Rais wa Bunge la Ulaya, Eva Kaili. Picha ya South China Morning Post.

Hata hivyo, ofisi ya waendesha mashtaka wa Ubelgiji haikutoa majina ya washukiwa hao wanne waliokamatwa lakini ilithibitishwa kuwa Eva Kaili ni miongoni mwa walioshitakiwa na wanne hao wameshtakiwa kwa makosa ya kujihusisha na mashirika ya kihalifu, utakatishaji fedha, na ufisadi.

Watuhumiwa hao, walikamatwa baada ya polisi na katika nyumba nyengine iliyopekuliwa inayoaminika kuwa ni ya Marc Tarabella, (Mbunge wa Ulaya wa chama cha kisoshalisti cha Uguriki na makamu mwenyekiti wa ujumbe wa bunge la Ulaya unaoshughulika na mahusiano ya rasi ya kiarabu), Tarabella ambaye bado hajashitakiwa.

Waendesha mashtaka wanasema, watu walio katika nafasi za kimkakati ndani ya bunge la Ulaya walilipwa pesa chungu nzima ili kushawishi uamuzi wa bunge kuelekea mjadala wa kisera wa Umoja wa Ullaya bila kuinyooshea kidole moja kwa moja Qatar.

Mkurugenzi, Afisa mipango wasimamishwa kazi
Rafiki wa Waziri Mkuu auawa kwa risasi