Mwili wa mwanafunzi wa Zambia, Lemekhani Nathan Nyirenda aliyefariki dunia wakati wa mapigano nchini Ukraine baada ya kuandikishwa katika jela ya Urusi umewasili uwanja wa ndege wa Lusaka, ambako ndugu na jamaa zake walikusanyika.

Mvulana huyo mwenye umri wa miaka 23, alikuwa akisomea uhandisi wa nyuklia katika Taasisi ya Fizikia ya Uhandisi ya Moscow lakini mwezi Aprili 2020 alihukumiwa kifungo cha miaka tisa na miesi sita jela kwa kosa la kutumia dawa za kulevya.

Lemekhani Nathan Nyirenda.

Wiki mbili baada ya Zambia kutaka taarifa, kundi la wanamgambo wa Urusi Wagner lilikiri kuwa lilimsajili kwa ajili ya operesheni maalum ya Moscow nchini Ukraine, na kusema alijiunga jeshini kwa hiari kabla ya kufa kishujaa.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Zambia, Stanley Kakubo alisema mapema mwezi huu kwamba sheria ya Urusi inaruhusu mfungwa kusamehewa mahsusi kwa operesheni maalum ya kijeshi.

Mwili wa mwanafunzi Mzambia, Lemekhani Nyireda katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda jijini Lusaka Desemba 11, 2022. Picha ya Salim Dawood / AFP.

Hata hivyo, Familia yake ilikataa kutoa maoni kwenye vyombo vya habari huku msemaji wa familia akisema mwili huo ulipaswa kuhamishiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti kwa ajili ya uchunguzi wa maiti hiyo na tarehe ya kuzikwa itatangazwa.

Try Again: Simba SC ipo katika mikono salama
Diamond, The Game mbioni kuachia 'goma jipya'