Rais Robert Mugabe amemfukuza kazi makamu wake Emmerson Mnangagwa kwa madai kuwa alionyesha tabia za kukosa uzalendo na uaminifu hasa kwa Rais.
Taarifa hizo zilizotolewa na waziri wa habari wa Zimbabwe Simon Kahaya Moyo ni ishara kuwa mke wa rais Robert Muabe, Bi Grace, atafuata nyayo za mumeme za kuwa rais wa Zimbabwe.
Awali mke wa rais Mugabe alitoa wito wa kutaka kutimuliwa kwa Mnangagwa kutoka katika chama cha Zanu-PF kabla ya kufanyika kwa mkutano wake wa mwezi ujao.
-
Mke wa Mugabe ataka makamu wa Rais afutwe kazi
-
Majaliwa ataka ujenzi wa shule ufanyike haraka
-
Afukuzwa kazi kwa kuuonyesha kidole cha kati msafara wa Trump
Akihutubia mkutano wa wanachama wa makanisa ya asili mji Harare siku ya Jumapili, Bi Mugabe alisema: “Nyoka ni lazima apigwe kwenye kichwa. Lazima tukabiliane na nyoka mwenyewe anayehusika na migawanyiko katika chama tunapoelekea kwenye mkutano tukiwa chama kimoja.”
Baada ya kufukuzwa kwa Mnangagwa nafasi hiyo inatarajiwa kujazwa na Bi Grace Mugabe na kuongeza uwezekano wa kumrithi mume wake.