Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameahidi kutoa kitita cha shilingi milioni moja kwa kila atakayesalimisha silaha yake ya moto kwa Jeshi la Polisi mkoani humo.

Makonda aliitoa ahadi hiyo jana alipokuwa akizungumza jijini humo na viongozi wa Halmashauri zinazounda mkoa huo.

Aliwahamasisha watu kurudisha silaha wasizozimiliki kihalali akiahidi kuwa hawatachukuliwa hatua yoyote ya kisheria na mahojiano ya wapi waliitoa hayatakuwa sehemu ya tatizo lao bali watazawadiwa kwa uamuzi huo wa kupunguza uhalifu.

“Atakayerudisha silaha yake kwa hiari atarumpa shilingi milioni moja. Hatutakuchukulia hatua yoyote, na usiwe na wasiwasi kuwa utaulizwa umetoa wapi… wewe sema tu umeikota,” alisema Makonda.

Mkuu huyo mpya wa Mkoa wa Dar es Salaam alisema kuwa hatua hiyo ni sehemu ya juhudi maalum za kuondoa uhalifu wa kutumia silaha na inaanza kwa hiari kwa kipindi maalum kabla hatua kali na msako mkali haujaanza dhidi ya wanaomiliki silaha kwa njia zisizo za halali.

 

 

Maalim Seif afunguka wakati wazanzibar wakipiga kura, ‘nasubiri rais atangazwe’
TCRA yawalinda Mke wa Rais Magufuli na Bi. Samia Suluhu Mtandaoni