Hatimae shirikisho la duniani FIFA limemaliza mzizi wa fitna kwa kupanga makundi ya fainali za kombe la dunia za 2018, zitakazounguruma nchini Urusi kuanzia Juni 14 hadi Julai 15.
Hafla ya upangaji wa makundi ya fainali hizo zinazosubiriwa kwa hamu kubwa na wadau wa soka ulimwenguni kote, zimefanyika State Kremlin Palace mjini Moscow nchini Urusi.
Kundi A: Russia, Uruguay, Egypt, Saudi Arabia
Kundi B: Portugal, Spain, Iran, Morocco
Kundi C: France, Peru, Denmark, Australia
Kundi D: Argentina, Croatia, Iceland, Nigeria
Kundi E: Brazil, Switzerland, Costa Rica, Serbia
Kundi F: Germany, Mexico, Sweden, South Korea
Kundi G: Belgium, England, Tunisia, Panama
Kundi H: Poland, Colombia, Senegal, Japan