Bao la Mshambuliaji kutoka DR Congo na Klabu ya Young Africans Fiston Kalala Mayele dhidi ya US Monastir limechaguliwa kuwa Bao Bora la wiki la Kombe la Shirikisho Barani Afrika katika mzunguuko wa Tano.
Mayele alifunga bao hilo na kuipa ushindi Young Africans wa 2-0 dhidi ya wawakilishi wa Tunisia katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, Jumapili (Machi 19).
Bao hilo limetangazwa kuwa kinara katika Mzunguuko watano, likiyashinda mabao mengine yaliyotajwa kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho yakifungwa na Ousimane Kamissoko wa AS Real Bamako dhidi ya TP Mazembe na Mydo Nakouho wa DC Motema Pembe dhidi ya ASEC Mimosas.
Kwa mantiki hiyo timu za Tanzania zimefanikiwa kuwa na mabao Bora mawili katika Mzunguuko watano, baada ya Bao la Kiungo wa Simba SC Clatous Chotta Chama alilolifunga dhidi ya Horoya AC kuchaguliwa kuwa Bao Bora upande wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.