Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya England, Gareth Southgate amesema Mshambuliaji na Nahodha timu hiyo Harry Kane amesahau yote baada ya matokeo mabaya kwenye Fainali za Kombe la Dunia.

Kane alikosa Penati katika mchezo wa Robo Fainali dhidi ya Ufaransa nchini Qatar, hivyo kuendeleza taifa hilo kusubiri kwa muda mrefu kutwaa taji hilo.

Kane angevunja rekodi ya kimataifa ya Wayne Rooney kama angefunga Penati hiyo na vilevile angeweza kuiongoza England kutinga nusu fainali, lakini akapiga shuti kali juu ya goli na wakapoteza kwa kufungwa mabao 2-1.

Hayuko peke yake katika maumivu ya moyo ya Penati kwa England, wachezaji wenzake Bukayo Saka, Marcus Rashford na Jadon Sancho wote wakikosa Penati katika Mchezo wa kichapo cha Penati dhidi ya Italia kwenye Uwanja wa Wembley wakati wa Fainali za Euro 2020.

Tukirudi nyuma zaidi, Southgate mwenyewe alikosa nafasi katika ushindi wa England katika Nusu Fainali dhidi ya Ujerumani kwenye michuano ya Euro 1996, kumaanisha Kane ndiye nyota wa hivi karibuni zaidi katika msururu wa nyota kupata maumivu ya moyo ya Penati.

Hata hivyo, Southgate anahisi hilo halitamrudisha nyuma mshambuliaji huyo wa klabu ya Tottenham na kumuunga mkono kama mmoja wa magwiji wa muda wote.

“Tumeona hilo kwa uchezaji wake na malengo yake kwa klabu yake,” amesema Southgate.

Heshima ya kuwa mfungaji bora wa mabao wa England inakaribia kumwangukia Kane, ambaye anafungana na Rooney mwenye mabao 53.

Robertinho aanza kuiwinda Raja Casablanca
Maleye afuata nyayo za Chama CAF