Saa chache baada ya kumaliza mchezo wa Mzunguuko watatu wa Kundi H wa kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2023’ dhidi ya Lesotho, kikosi cha Zambia ‘Chipolopolo’ kimefanya safari na kuwasili salama Afrika Kusini, tayari kwa mchezo wa Mzunguuko wanne wa Kundi hilo.

Timu hizo zitarudiana tena Keshokutwa Jumapili (Machi 26) katika Uwanja wa Dobsonville mjini Johannesburg Afrika Kusini, huku Lesotho ikiwa mwenyeji wa mchezo huo.

Zambia imewasili Afrika Kusini ikishabihishwa na ushindi wa mabao 3-1 uliopatikana jana Alhamis (Machi 23) katika Uwanja wa Levy Mwanawasa, mjini Ndola, huku mabao yakifungwa na Fashion Sakala, Lameck Banda aliyefunga mawili dakika ya 37, 53 na 57, huku  Tshwarelo Bereng akiitanguliza Lesotho dakika 33.

Ushindi huo umeiweka kileleni Zambia kwa kufikisha alama 06, huku ikisubiri matokeo ya mchezo mwingine wa Kundi hilo kati ya Ivory Coast itakyokuwa mwenyeji wa Comoros katika Uwanja wa Bouaké, mjini Bouaké.

Ivory Coast ipo nafasi ya pili baada ya kucheza michezo miwili na kukusanya alama 04, huku Comoro ikiwa nafasi ya tatu kwa kufikisha alama 03 na Lesotho inabuza mkia baada ya kujikusanyia alama 01.

Kibarua asimulia alivyoweza kumiliki Hoteli ya nyota tano
Tshabalala aitakia kheri Taifa Stars