Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa amewasisitiza Madiwani wa Halmashauri kuendeleza jitihada za usimamizi wa usafi katika Jiji la Mbeya, kutokana na uwepo wa changamoto za ukusanyaji taka kwa wazabuni waliopewa tenda.

Malisa ameyasema hayo wakati akitoa salamu za Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera kwenye Baraza hilo, na kusema ufanisi katika ukusanyaji taka ni lazima uongezwe kabla hatua stahiki hazijaanza kuchukuliwa.

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa.

Kwa upande wake Afisa Usafi Wa Mazingira Jiji la Mbeya, Nimrod Kiporoza amesema wako tayari kutekeleza maagizo hayo na tayari mikakati imewekwa ili kuwawajibisha wazabuni watakaokiuka makubalino ya kusanyaji taka.

Eguma: Hatutacheza kinyonge, tutapambana
Arsenal yahofiwa kurudia kosa