Mjane wa aliyekuwa Rais wa awamu ya Tano wa Tanzania, Hayati John Magufuli, Mama Janeth Magufuli ametunukiwa Tuzo ya heshima ya Kimataifa inayotolewa na taasisi ya Martha Tshisekedi Kasalu maarufu M. T. Kasalu ikilenga kutambua mchango wake kwa Taifa na alioutoa kwa mwenza wake.

Tuzo hiyo ya M. T. Kasalu, Femme D’Honneur Trophee, ilitolewa kwa Mama Janeth Magufuli Machi 24, 2023 jijini Kinshasa, DRC na hutolewa kwa wenza  wa viongozi wakuu wa nchi na watu maarufu Duniani, kwa kutambua michango yao kwa wenza wao, jamii na taifa husika.

Mama Janeth Magufuli, akiwa ameshikilia tuzo yake ya M. T. Kasalu, Femme D’Honneur Trophee.

Wengine waliopokea tuzo hiyo ni pamoja na  mke wa daktari maarufu nchini humo (DRC), Mama Suzanne Mukay muhusika wa magonjwa ya kina mama na kansa, ambaye mumewe ameisaidia jamii kwenye sekta hiyo na mke wa Mchungaji maarufu nchini DRC, Roland Dalo, Mama Vivianne Daloaliyeisaidia jamii hasa wajane, yatima na vijana kujitegemea.

Zoezi la kukabidhi tuzo kwa Mama Janeth Magufuli, lilivyokuwa likiendelea jijini Kinshasa – DRC.

Mwingine ni Mama Colette Senghor, mke wa Rais wa kwanza wa Senegal, Leopold Sedar Senghor, alieisaidia Senegal kupata uhuru na mama Coretta King, mke wa Martin Luther King, ambaye mumewe anatajwa kusaidia kupinga ubaguzi wa rangi nchini Marekani.

Sehemu ya washindi wa tuzo hizo zilizotolewa na Taasisi ya LIZADEEL kwa kushirikiana na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Urithi ya DRC.

Tuzo za M. T. KASALU hutolewa na Taasisi ya LIZADEEL kwa kushirikiana na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Urithi ya DRC, UNESCO, UN-WOMEN na Asasi za Kiraia na Mama Janeth Magufuli alikua ni mmoja kati ya wanawake 150 waliokuwa wamependekezwa kuziwania.

Mwaibula: Mteule wa Mkapa, mwanzilishi ruti za Daladala
Serikali yataka ushahidi matukio ukatili wa kijinsia