Shujaa wa filamu ya Hotel Rwanda, Paul Rusesabagina, ambaye pia alikuwa ni mkosoaji mkubwa wa Serikali ya Rais wa Rwanda, Paul Kagame anatarajia kuachiliwa huru baada ya taratibu zote za kisheria kukamilika.

Msemaji wa serikali ya Rwanda, Alain Mukuralinda amesema Rusesabagina aliwahi kuhukumiwa kwa sababu alistahili na kwamba kwasasa hakuna shaka kua anatakiwa kuwa huru kwakuwa sheria inaruhusu.

Amesema, “hakuna shaka kwamba utaratibu huo uliheshimiwa, tukumbuke kwamba ukirudia tena na tena makosa yale yale, unarudi kwenye hukumu na kwa upande mwingine kwa wahasiriwa, ikiwa ulipigwa faini, basi faini zinabaki ila sasa atakuwa huru.”

Shujaa wa Filamu ya Hotel Rwanda, Paul Rusesabagina. Picha ya Africanews.

Taaarifa hiyo, imekuja ikiwa ni siku moja baada ya Rais Kagame kuondoka Qatar, ambako serikali yake inatafuta njia za kutatua kesi hiyo iliyokuwa chanzo cha wasiwasi kwa nchi za Magharibi na wanaharakati wa haki.

Rusesabagina, ambaye pia alishiriki katika filamu maarufu ya Hotel Rwanda, alifungwa jela kwa mashtaka ya ugaidi Septemba 2021 na familia yake imezishutumu mamlaka kwa kumtesa na kuonya kuhusu kuzorota kwa afya yake.

Fiston Mayele apeleka salamu TP Mazembe
Simba SC: Tunaenda kusaka heshima Morocco