Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amewataka viongozi kujitathmini katika chaguzi kama wamepita kwa rushwa au weledi ambapo amesema kiongozi mzuri ni yule anaye pita rushwa mjitathimini mkishindwa kujipanga huko juu tutawapanga.
Akihutubia katika Baraza kuu la Umoja wa wanawake, UWT, lilofanyika leo Agosti 10, 2020 Jijini Dodoma, amesema anatumaini viongozi wote waliopita kwenye mchujo hapo awali ni viongozi bora ambao sio wapokeaji wala watoaji rushwa.
”Jukumu la kulainisha mchakato limeachwa kwenu UWT, hivyo mnatakiwa kujitoa hasa,jukumu lililopo mbele yenu ni zito na sio jepesi kama mnavyodhania”, amesema Makamu wa Rais
”Kiongozi mzuri ni yule ambaye anapata uongozi kwa weledi bila rushwa, anayejiamini sasa mjitathimini mkishindwa kujipanga huku chini huko juu tutawapanga”, amesema Makamu wa Rais