Klabu ya Manchester City inaamini ujio wa kocha Pep Guardiola, huenda ukamshawishi mshambuliaji hatari kutoka nchini Argentina na FC Barcelona, Lionen Adres Leo Messi, kujiunga na klabu hiyo ya Etihad Stadium.

Licha ya kudhibitisha kwake juu ya kutokuwa na mpango wa kuihama FC Barcelona inaamini kwamba ujio wa meneja huyo kutoka nchini Hispania, utamvutia ikizingatia kwamba amekuwa na kashfa ya ukwepaji wa kodi.

Hata hivyo Manchester City, italazimika kutoa kitita kikubwa cha fedha endapo itahihitaji kwa dhati huduma ya mshambuliaji huyo aliyetengeneza muunganiko mzuri wachezaji wengine huko Camp Nou akiwepo Luis Suarez na Neymar.

Lionel Messi aliwahi kukaririwa akikana kuwa na nia ya kuihama klabu ya Barcelona yenye maskani yake Katulanya.

Stars Kurejea Dar Usiku Wa Manane
Raheem Sterling Kuwa Shuhuda Mpaka Mwishoni Mwa Msimu