Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhandisi, Stella Manyanya amefungua kikao cha siku tatu mjini Dodoma kwa njia ya Mtandao (Video Conferece) huku akiwataka wataalam katika ngazi ya Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa kutumia mwanya huo kubadilishana uzoefu.
Amesema kuwa wanatakiwa kuutumia mwanya huo kuibua fursa zilizopo katika maeneo yao, uanzishwaji na uendelezaji wa viwanda vidogo, vyakati na vikubwa ifikapo 2025.
Manyanya amesema kuwa kupitia fursa ya Viongozi hao wa Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kukutana kwa njia ya Mtandao kutawezesha wote kuwa na uelewa wa pamoja kuhusu mikakati ya ujenzi wa Uchumi wa Viwanda
“Mkutano huu utatusaidia pia kupambanua mikakati ya kufufua viwanda vilivyokufa na namna nzuri ya kupata wawekezaji wapya,”amesema Manyanya.
-
Mawakili watakiwa kujiajiri
-
Ndugai: Lissu tunampenda sana, nitakwenda kumuona
-
Benki za Wananchi zawekwa mtegoni
Hata hivyo, Manyanya ameongeza kuwa katika awamu ya kwanza Wakala wa Usajili Biashara na Leseni (BRELA), watatoa mafunzo juu usajili wa Biashara, Miliki, Ubunifu sambamba na ujenzi wa uchumi wa Viwanda kama falsafa ya Rais wa awamu ya tano inavyojiapambanua kuhusu suala zima la viwanda.