Kwa mara ya kwanza Mkuu wa Idara Ya Habari na Mawasiliano ya Simba SC Haji Manara ametoa maoni kuhusu usajili wa kuelekea msimu mpya wa ligu 2021/22.
Manara alikua kimya tangu tetesi za usajili zilipoanza kuchukua nafasi katika mitandao ya kijamii na kwenye baadhi ya vyombo vya habari.
Mdau huyo ambaye amekua sehemu ya kunogesha soka la Tanzania kupitia nafasi alionayo Simba SC, mara nyingi anapozungumzia usajili huwa anaichokonoa Youbg Africans ambayo kwa msimu wa nne mfululizo imekua na wakati mgumu kwa kushindwa kutwaa taji la Ligi Kuu.
Manara amewasilisha mtazamo wake wa usajili katika kiopindi hiki kwa kuandika katika kurasa zake za mitandao ya kijamii.
Ameandika: Tunakaribia kuingia katika Dirisha kubwa la Usajili wa wachezaji kwa ajili ya msimu wa 2021/22 na kuendelea.
Kama kuna kipindi sikifurahii kikazi ni hiki, huku ikitumika lugha halali ya ‘TETESI’ kwangu kinakuwa kipindi kigumu sana toka kwa washabiki na hata waandishi wa habari !!
Yes kwa kutumia neno tetesi utasikia Simba kumsajili Djuma Ramadhani au Baba Tunde toka El Merekh au Mzungu wa kaizer kutua Msimbazi !!
Mitandao ya kispoti, baadhi ya Tv, Redio na Magazeti wanayo hiyo haki ya kuandikwa hcho kiitwacho tetesi , shida yangu ni pale tetesi zisizotokana na vyanzo vya klabu kupigiwa simu mimi kuulizwa kuhusiana na kina Baba Tunde na porojo nyingine za kitetesi
Sasa kumi ni pale washabiki wanapokuwa na matarajio kwamba tumemsajili flani au flani, na hapo shida inakuja usajili ushafungwa halafu huyo Djuma wa tetesi hayupo kikosini.
Mitandaoni lawama zinaujia uongozi kisa tetesi zetu!!
Hope msimu huu tutaendelea na tetesi bila kutaka uthibitisho wetu na bila shaka Washabiki wetu washaujua mfumo na taarifa zetu kuhusu usajili ,,nn tunafanya.
Tuendelee na tetesi zetu coz ndio soko lilivyo ila maneno yangu ndio hayo