Shirika la Afya Duniani WHO, limesema idadi ya vifo kutokana na vita vibaya vya takriban mwezi mmoja nchini Sudan sasa ni zaidi ya watu 600.

WHO imesema zaidi ya watu 5, 000 wamejeruhiwa kutokana na mapigano hayo baina ya jeshi la Sudan na kikosi cha RSF huku makubaliano ya kusitisha mapigano yakishindwa kumaliza mzozo na kupunguza ghasia .

Umoja wa Mataifa UN, umesema mlipuko wa mapigano Sudan unataabisha hali ya kibinadamu huko eneo la Abyei, lililopo katika mpaka wa Sudan Kusini na Sudan.

Mwakilishi wa umoja wa mataifa katika umoja wa Afrika, Hanna Serwaa Tetteh amesema hali ya ukosefu wa usalama mpakani baina ya Sudan na Sudan Kusini inaweza kuongezeka wakati wa harakati za kuvuka mpaka kwa makundi yenye silaha na ya uhalifu.

Aidham Tetteh ameongeza kuwa, mapigano nchini Ssudan pia yanaathiri shughuli za kibiashara za kila siku na usambazaji wa chakula na bidhaa nyingine muhimu kutoka Sudan kwenda Sudan Kusini na kuhatarisha uuzaji wa mafuta kutoka kusini.

Bares awapongeza wachezaji Tanzania Prisons
Watatu kusajiliwa Azam FC 2023/24