Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Rex Tillerson yupo ziarani barani Afrika, ikiwa ni ziara yake ya kwanza ambapo atazitembelea nchi za Chad, Djibouti, Ethiopia, Nigeria na Kenya.

Tillerson atawasili mapema hii leo nchini Ethiopia, nchi ambayo uchumi wake unakua kwa kasi ingawa bado inakabiliwa na mgogoro wa kisiasa.

Aidha, akiwa nchini humo Tillerson atakutana na viongozi wa ngazi za juu wa Ethiopia kujadili mchakato wa kumpata atakayechukua uongozi na kuangalia namna ya kutatua vurugu za kisiasa zinazoendelea kujitokeza.

Hata hivyo, baada ya Ethiopia, atazitembelea nchi za Kenya, Nigeria, Chad na Djibouti ambapo Marekani inaona kuwa ni washirika wake wa karibu wa kupambana na Ugaidi na kuleta usalama wa kikanda.

 

 

 

 

 

 

Video: Mangula awachana wanasiasa wachochezi, Mbowe alazwa awekwa oxygen
Aiba tuzo ya Oscar ya Muigizaji bora wa kike, polisi wapambana