Mwanaume mmoja ambaye jina lake halijafahamika huko nchini Marekani katika mji wa Washington, amejifyatulia risasi nje ya Ikulu ya Marekani (White House) na kufariki dunia.

Tukio hilo limethibitishwa kutokea na kikosi cha kumlinda Rais ambao wameshuhudia kutokea kwa tukio hilo, na wamesema kuwa, mwanaume huyo kabla ya kujiua alifyatua bunduki mara kadha akiwa nje ya Ikulu katika barabara ya Pennsylvania.

Ijapokuwa alikuwa kwenye watu wengi wakati akijipiga risasi, Kikosi cha ulinzi wa Rais kimesema kuwa, hakuna mtu hata mmoja aliyejeruhiwa, kwani watu waliozunguka eneo hilo mara baada ya kusikia kelele za mlio wa risasi walisambaratika na kukimbia eneo hilo mara moja.

Hata hivyo Rais wa nchi hiyo, Donald Trump hakuwa kwenye Ikulu yake , bali alikuwa katika kasri lake la Mar-a-Lago huko Florida.

Bado haijafahamika zaidi kwa nini kijana huyo aliamua kuchukua uamuzi huo, upepelezi wa kina unaendelea kufanyika nawahusika wa katika kitengo hiko kujua chanzo cha cha kushiriki kosa hilo la jinai na kujisababishia kifo.

Aidha hivi karibuni nchini Marekani kumeripotiwa matujio ya kadha wa kadha yanayohatarisha usalama katika Ikulu ya White House.

 

Museveni awatumbua Mkuu wa Polisi, Waziri wa Ulinzi kukomesha utekaji
Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Machi 5, 2018