Marekani imeyataka mataifa yote kuvunja uhusiano wa kidiplomasia na wa kibiashara na Korea Kaskazini baada ya taifa hilo kufanya jaribio la kombora lake la masafa marefu.
Akizungumza katika baraza la usalama la umoja wa kimataifa ,mjumbe wa Marekani katika baraza hilo, Nikki Haley amesema kuwa rais Trump amemtaka mwenzake wa China kukata usambazaji wa mafuta Korea Kaskazini
Aidha, amesema kuwa Marekani haitaki mzozo lakini Korea Kaskazini itaangamizwa kama vita itazuka katika ukanda huo.
Hata hivyo, hayo yanajiri baada ya Korea Kaskazini kurusha kombora siku ya Jumatano ambalo liliruka kilomita 4,475, ikiwa ni mara kumi zaidi ya kimo cha kituo cha angani.