Marubani wawili, injinia Edger Alfred Mcha (26) na Dominic Bomani (64) wamefariki dunia papo hapo katika ajali ya ndege iliyotokea Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar walipokuwa wakiifanyia majaribio ya kuruka wakati wa matengenezo.

Katika uchunguzi uliofanywa jana Saa 12:45, Daktari bingwa wa uchunguzi Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Zanzibar, Dk Msafiri Marijani amesema wamebaini kuwa vifo vya marubani hao vimesababishwa na kukosa hewa safi wakati wa ajali na kuathiriwa na moto

Mhandisi Mkuu wa Kampuni ya Tropical Air, David Kisusi amesema ndege hiyo ilianguka na kuungua jana, Alhamisi Februari Mosi saa saba mchana.

Aidha ameongezea kuwa ndege hiyo aina ya 5H-TDF yenye uwezo wa kubeba abiria wanne ni mali ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) iliyokuwa Zanzibar kwa matengenezo.

Amesema kwa takriban miezi sita ndege hiyo ilikuwa uwanjani hapo kwa matengenezo.

“Tulikuwa tunaijaribu baada ya matengenezo, iliporuka tu ilianguka na kulipuka, marubani wetu wamefariki dunia,” amesema Kisusi leo Februari 2, 2018.

Mtoto wa Fidel Castro ajiua
Ujumbe wa mwisho wa Zari kabla ya kum-unfollow Diamond