Mashabiki wa Klabu Bingwa Duniani Real Madrid, wameanzisha Kampeni ya kutaka kumuondoa Klabuni hapo Mchezaji wao David Alaba, kufuatia kitendo cha kumpigia Kura Lionel Messi.
Imethibitika wazi Alaba alimpigia Kura Messi, ambayo imechangia Mshambuliaji huyo wa Argentina na Klabu ya PSG ya Ufaransa, kushinda Tuzo ya Mchezaji Bora 2022 wa FIFA, akiwashinda Kylian Mbappe na Karim Benzema.
Mashabiki hao wa Real Madrid wanaamini kitendo kilichofanywa na Alaba ambaye ni Nahodha wa Timu ya taifa ya Austria, kimedhihisha usaliti dhidi ya Mshambuliaji wao Benzema ambaye ameshika nafasi ya pili, huku ya tatu ikienda kwa Kylian Mbappe.
Kupitia Akaunti za Mtandao wa Twitter Mashabiki hao wamekuwa wakindika #AlabaOut, pia kwenye Post zake za Instagram wamekuwa waki-comment kwenye comments Kwa kuandika #AlabaOut.
Mwaka 2012 Alaba aliwahi kuonesha Mapenzi yake ya wazi wazi Kwa Lionel Messi, ambapo alipost maelezo ya picha ‘Caption’ yaliyokuwa yanaashiria furaha Baada ya Messi kufunga goli.
Hata hivyo sakata hilo bado halijatolewa taarifa na kiongozi yoyote, huku ikiaminiwa mkataba wa Alaba na Real Madrid unaendelea kuheshimiwa licha ya mihemko kuendelea kwa baadhi ya Mashabiki.
Alaba alisajiliwa Real Madrid mwishoni mwa msimu wa 2020/21 akitokea kwa mabingwa wa Soka wa Ujerumani FC Bayern Munich, huku akiitumikia Klabu hiyo ya mjini Madrid katika michezo 49 na kufunga mabao matatu.