Maelfu ya mashabiki wa Lionel Messi wamepigwa na butwaa baada ya kusafiri umbali mrefu kwenda kumuona staa huyo huko Atalanta, hata hivyo, alibaki Miami huku Inter Miami ikipokea kichápo cha 5-2 dhidi ya Atalanta United.

Kuelekea mchezo wa Inter Miami na Atalanta United kabla ya kuchezwa maelfu ya jezi za pinki za Messi zilienea nje ya uwanja hata hivyo, staa huyo hakucheza kutokana na kuwa majeruhi.

Gazeti la Dail Mail lilizungumza na mashabiki waliokuwa nje ya Uwanja wa Mercedes-Benz, wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 73,000 walidai walisafiri umbali mrefu kwa ajili ya kumuona Messi bila kujua hakujumuishwa kikosini.

Familia moja iliendesha gari saa 10 kutoka Florida Kusini kwa ajili ya mechi hiyo huku mashabiki wengine wakinunua tiketi za gharama kwa ajili ya mechi hiyo ya ligi.

Awali ilitarajiwa Messi angecheza mechi hiyo lakini picha ziliibuka mtandaoni akimwangalia mtoto wake akiichezea timu ya vijana ya Inter Miami.

Tiketi za mechi hiyo ziliuzwa wiki kadhaa zilizopita, huku wafanyakazi wa Atlanta United wakiweka viti vya ziada kwa ajili ya mechi hiyo.

Hersi Said: Hili ndilo tunalolitaka sasa
Azam FC yaivutia kasi Singida Fountain Gate