Kikosi cha Young Africans kimesaliwa na saa kadhaa za maandalizi kabal ya kuwakabili Al Merikh ya Sudan huku Wananchi hao wakiwa na lengo la kupata ushindi katika Uwanja wa ugenini.

Mbali na ushindi wa ndani ya Uwanja, lengo lingine la Wananchi ni kuhakikisha kuwa wanautawala mchezo huo kuanzia kwa mashabiki ambao watachagiza mpango wa kuondoka katika Uwanja wa ugenini wakiwa na matokeo mazuri.

Katika kuthibitisha hilo mashabiki zaidi ya 1000 ambao wamesafiri kuelekea nchini Rwanda wameuteka mji wa Kigali kuanzia leo Ijumaa (Septemba 15).

Tayari mashabiki hao wameshawasili mjini Kigali-Rwanda leo ljumaa (Septemba 15) huku kikosi cha Yanga chenyewe kikiwasili tangu jana Alhamisi (Septemba 14) tayari kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo.

Young Africans wanatarajiwa kuwa wageni wa Al Merrikh katika mchezo unaotarajiwa kufanyika kesho Jumamosi (Septemba 16) katika Uwanja wa Kigali Pele uliopo Kigali, Rwanda.

Ofisa Habari wa Young Africans, Ally Kamwe amesema: “Kwa sasa tumeshawasili nchini Rwanda tayari kwa ya maandalizi ya mchezo wetu.

“Niwahakikishie kuwa kikosi chenyewe kimeshawasili Rwanda kabla yetu na wachezaji wametuahidi kuwa wanaenda kupata matokeo mazuri.

“Leo tukiingia Rwanda mji wote tutauteka sisi Wananchi kuonyesha kuwa tunahitaji jambo letu,” amesema kiongozi huyo.

Wahitimu la Saba watakiwa kudumisha Nidhamu Mtaani
Waliosababisha vifo watu sita wasakwa na Polisi