Jeshi la Nigeria limesema kuwa zaidi ya watu 700 waliokuwa wanashikiliwa na kundi la wapiganaji wa Boko Haram kaskazini mashariki mwa nchi hiyo wamefanikiwa kutoroka.

Msemaji wa jeshi Kanali, Timothy Antigha amesema kuwa wamefanikiwa kutoroka kupitia visiwa kadhaa vya ziwa Chad na kufanikiwa kufika katika mji wa Monguno katika jimbo la Borno.

Aidha, Jeshi hilo limesema kuwa operesheni zilizofanywa hivi karibuni zimelidhoofisha nguvu kundi hilo la Boko Haram.

Hata hivyo, katika Hotuba yake ya mwisho wa mwaka rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari amesema kuwa kundi hilo limekwisha sambaratishwa.

 

Video: Vigogo 180 kitanzini Takukuru, Makonda sasa kugharamia mkesha wa mwaka mpya
Rouhani: Trump ni adui namba moja wa Iran