Mauaji ya kutumia Silaha yameendelea kujitokeza Wilaya ya Rufiji, Kibiti na Mkuranga mkoa wa Pwani mara baada ya Katibu ya CCM Kata ya Bungu Wilayani Kibiti, Halife Mtulia kuuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiofahamika.
 
Hayo yamesemwa na Katibu wa CCM wilaya ya Kibiti, Zena Mgaya ambapo amesema kuwa marehemu aliuawa akiwa anatoka uwani nyumbani kwake kwenda kuoga ndipo walipojitokeza watu wawili na kumfyatulia risasi kisha kutokomea kusikojulikana.
 
“Wauaji hao walitumia usafiri wa pikipiki kwa kuiacha mbali na eneo la tukio na baada ya kutimiza adhma yao walitembea kuifuata walipo ipaki kisha kuondoka,“amesema Mgaya.
 
Kwa upande wao Wananchi wamesema hali bado ni mbaya sana wilayani humo, hivyo wameliomba jeshi la polisi bkuongeza ulinzi ili kuweza kukomesha matukio ya kikatili kama hayo.
 
Hata hivyo, Zena amesema kuwa kufuatia matukio ya mauaji kijiji cha Nyambunda kata ya Bungu kimeshapoteza Mwenyekiti wa kiiji, Mtendaji wa Kijiji, na wenyeviti watatu wa vitongoji vilivyoko katika kijiji hicho

Prof. Mukandala awaasa vijana, Asema utu, maendeleo na maisha bora havipatikani kwa fedha
Fainali za AFCON U-17 kuanza kutimua vumbi leo