Licha ya kuwa kwenye hati hati ya kupoteza nafasi ya kurudi uraiani tangu akutwe na hatia ya mashtaka ya unyanyasaji wa kingono yanayomkabili., Mauzo ya muziki wa msanii kutoka nchini Marekani R. Kelly yameripotiwa kupanda kwa asilimia 517.
Kwa mujibu Rolling Stone chats, wameripoti kuwa mauzo ya muziki wa R.Kelly kwenye digital platforms mbali mbali yameendelea kupanda kwa kasi kutoka 11.2 Milioni mpaka 13.3 Milioni, ndani ya wiki moja tangu mahakama kuthibitisha kuwa imemkuta na hatia ambayo pengine hukumu yake inaweza mpeleka gerezani kwa miaka 10 au kifungo cha maisha.
Mashtaka hayo ya Unyanyasaji wa Kingono ni jambo lililopelekea baadhi ya Mitandao ikiwa ni pamoja #Youtube #AppleMusicĀ #Spotify na mingine kuziondoa kazi zake kama sehemu ya kuiunga mkono mahakama na kukemea shutma zinazomkabili.
Inaelezwa hata baadhi ya wasanii kama Celin Dion, Lady Gaga na Chance the Rapper, wao walimuondoa R Kelly kwenye nyimbo walizofanya pamoja kipindi cha nyuma.
Robert Kelly anatuhumiwa kufanya unyanyasaji wa Kingono kwa wanawake kwa kuwalaghai kupitia umaarufu na kipato chake na hata wengine kwenda mbele zaidi wakisema amekuwa akiwalazimisha kufanya ngono za wao kwa wao kama sehemu ya unyanyasaji.