Mshambuliaji wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Fiston Kalala Mayele amesema kuwa wapo katika mipango imara kuhakikisha wanapata ushindi dhidi ya Marumo Gallants ili kuongeza kasi ya kuwania Ubingwa wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Young Africans inatarajia kushuka kwenye Uwanja wa Royal Bafokeng kesho Jumatano (Mei 17) kupambana na Marumo Gallants, huku mchezo huo unatarajiwa kuwa na upinzani mkubwa licha ya kuwa mbele kwa mabao 2-0.

Mayele, ambaye hadi sasa amepachika mabao matano akishika nafasi ya kwanza katika orodha ya wafungaji sambamba na Ranga Chivaviro, kila mmoja amepachika mabao matano, amesema hivi sasa akili yake ipo katika mchezo wa Marumo Gallants, ambao ni muhimu kwao ili kujiweka katika hatua nzuri ya kutinga hatua ya Fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

“Tuko vizuri na tunaendelea na mazoezi kwa ajili ya mchezo ujao, nipo hapa kuipambania timu yangu pamoja na kutimiza malengo yangu ya kutwaa kiatu cha ufungaji bora,” amesema Mayele

Young Africans wanaingia katika mchezo huo wakiwa tayari wametetea taji la Ligi Kuu Bara baada ya kuifunga Dodoma Jiji FC mabao 4-2 kwenye Uwanja wa Azam Complex.

TASWA yarudisha Tuzo ya Mwanamichezo Bora
Vifo vya mfungo tata: Miili iliyofukuliwa sasa ni zaidi ya 200