Baada ya kustaafu masumbwi bila kuonja kipigo, bingwa wa zamani wa masumbwi duniani, Floyd Mayweather amethibitisha kuanza mazoezi ya kushiriki pambano la ngumi, mateke na viwiko yanayofahamika kama UFC/MMA.
Mayweather ameiambia TMZ kuwa ataanza rasmi mazoezi baadaye mwaka huu chini ya mkufunzi ambaye ni bingwa wa zamani wa UFC, Tyron Woodley.
“Nitaanza hivi karibuni. Tumekuwa tunawasiliana kwa jumbe za simu mara kwa mara. Tumezungumza kuhusu hilo mara kadhaa, tutaanza rasmi mazoezi hivi karibuni,” alisema Mayweather mwenye umri wa miaka 41.
Mwaka jana, bondia huyo alirejea kwenye ulingo wa masumbwi na kumpiga bingwa wa michezo ya MMA/UFC, Conor McGregor katika pambano lililofanyika Las Vegas, Marekani.
- Mtoto wa Jay Z atisha mnadani, aweka dau la $19,000
- Taesa yatoa ufafanuzi jinsi ya kujisajili ajira 10,000 bomba la mafuta Hoima
Pambano hilo lilimfanya Mayweather kuweka rekodi ya kushinda mapambano yake yote 50.