Jeshi la Polisi Mkoani Songe linamshikilia Dereva wa bajaji katika mji wa Vwawa wilayani Mbozi, Ayubu Mng’osi (30) kwa tuhuma za kubaka na kufanya shambulio la aibu kwa watoto wawili wenye umri wa miaka 7 na 9 ambao ni wanafunzi wa shule ya  msingi.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Theopista Mallya amesema alisema katika tukio la kwanza, mtuhumiwa huyo anadaiwa kumwingilia kimwili mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya Msingi Ichenjezya.

“Mbinu aliyoitumia mtuhumiwa ni kumlaghai mtoto na kuingia naye ndani ya nyumba anayoishi kisha kumwingilia kimwili,” amesema Kamanda Theopista Mallya.

Aidha, amebainisha kuwa mtuhumiwa huyo pia anadaiwa kumfanyia shambulio la aibu la kumshika na kumchezea sehemu za siri mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya Ichenjezya Wilayani Mbozi na tukio hilo lilifanyika Julai 14, 2023.

Maji yaibua shangwe Buhigwe, Aweso amkubali Mkandarasi
Rais Samia amshika mkono mama mkumbatia watoto