Hatma ya mabingwa wa soka nchini England Manchester City kushiriki michuano ya klabu bingwa barani Ulaya na Europa League itafahamika juma hili, kufuatia rufaa yao kupangwa kusikilizwa kwenye Mahakama ya Usuluhishi Michezoni (CAS).

Leo Jumatatu klabu hiyo iliyo chini ya wamiliki kutoka wa Saudi Arabia itaanza kutoa pingamizi mahakamani hapo, juu ya kupinga adhabu ya kufungiwa kushiriki michuano ya barani Ulaya kwa miaka miwili, iliyotangazwa na Shirikisho la Soka Barani humo UEFA.

Februari 14 mwaka 2020, Bodi ya Usimamizi ya Fedha za UEFA (CFCB) iliifungia klabu ya Manchester City kushiriki michuano ya UEFA kwa miaka miwili, sambamba na kulipa faini ya Euro milioni 30 baada ya kubainika kuwa na matumizi mabaya ya fedha katikati ya mwaka 2012-2016.

Aidha, Bodi ya Usimamizi ya Fedha za UEFA (CFCB) imesema licha ya pingamizi la City lakini Bodi hiyo imesema klabu haikutoa ushirikiano wa kutosha katika uchunguzi wa matumizi ya fedha.

Pingamizi hilo litasikilizwa na wanasheria watatu wa CAS, ambapo itafanyika katika kikao cha siri kwa njia ya video kwa siku tatu mfululizo na majibu ya pingamizi hilo yanaweza kutolewa baadae msimu huu.

Bila kushinda mashtaka hayo, klabu ya Manchester City haitashiriki michuano ya Ulaya kwa msimu ujao, watazuiliwa pia kucheza michezo ya fainali ya UEFA Super Cup hata kama watashinda taji la UEFA msimu huu.

Rais wa La Liga Javier Tebas, ambaye awali alizituhumu klabu za Manchester City na Paris Saint Germain kuwa na matumizi mabaya ya fedha, anaamini kuwa FFP itafuata sheria kwenye kuamua hilo.

Serikali yaanza biashara ya Mafuta
Uingereza: Sanamu ya mfanyabiasha wa utumwa yavunjwa kupinga ubaguzi