Mabingwa wa soka Tanzania bara Simba SC leo asubihi wamecheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Transit Camp inayoshiriki ligi daraja la kwanza Tanzania bara.

Mchezo huo umechezwa kwenye uwanja wa mazoezi wa mabingwa hao (Mo Simba Arena) uliopo Bunju jijini Dar es salaam, na kushuhudia Simba wakichomoza na ushindi wa mabao manne kwa mawili.

Mabao ya Simba yalifungwa na Deo Kanda dakika ya tatu, Gerson Fraga dakika ya 15, Tairone Santos dakika ya 17 na Meddie Kagere dakika ya 46.

Mabao mawili ya kufutia machozi kwa upande wa Transit Camp yalifungwa na Hamadi Habibu dakika ya 45 na Nisile Kisimba dakika ya 64.

Huo ni mchezo wa kwanza wa kirafiki kwa Simba SC tangu waliapoanza maandalizi ya kuendelea na ligi kuu majuma mawili yaliyopita chini ya kocha Sven Vander Broeck.

Hata hivyo leo jioni Simba SC watacheza mchezo wa pili wa kirafiki dhidi ya KMC kwenye uwanja wa Mo Simba Arena, ikiwa ni muendelezo wa maandalizi, kabla ya kuendelea kwa michezo ya ligi kuu mwishoni mwa juma hili.

KMC watacheza mchezo huo huku wakiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa mabao matatu kwa sifuri walioupata dhidi ya Young Africans jana Jumapili Uwanja wa Uhuru, Dar es salaam.

Mpina atangaza kibano waingizaji haramu wa maziwa
Man Utd na Real Madrid zagongana kwa Lautaro Martinez