Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema kuwa wao wanatoa taarifa ya maendeleo ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kulingana na madaktari wanavyowaambia.
Amesema kuwa wao hawawezi kusema chochote nje ya wataalam hao ambao ndio wenye ujuzi wa kumtibu na kujua hali ya mgonjwa kwa kuwa ndiyo watu ambao wanakaa naye muda mrefu na kutambua maendeleo yake.
“Sisi tunatoa taarifa za maendeleo ya Lissu kulingana na Madaktari wanavyotuambia, hatuwezi kusema chochote nje ya wataalam hao, kwa kuwa ndio wenye ujuzi wa kumtibu na kujua maendeleo ya mgonjwa husika, Unajua ahueni humtokea mgonjwa taratibu taratibu na ndivyo inavyotokea kwa Lissu, ingawa sisi wote tuna hamu apone mara moja aje aendelee kupigania haki za wanyonge kama alivyokuwa akifanya,”amesema Mbowe
Aidha, amewaomba Watanzania kuzidi kumuombea Tundu Lissu na kuendelea kuchangia gharama za matibabu kwa kiongozi huyo kwani gharama za matibabu yake ni kubwa na wao kama chama peke yao hawawezi.
-
Nyalandu aweka kambi Nairobi kusubiri ruhusu ya kumpeleka Lissu Marekani
-
Kubenea atua Dodoma kuhojiwa
-
Video: JPM aagiza kujengwa uzio kulizunguka eneo la Mererani
Hata hivyo, Tundu Lissu yupo Jijini Nairobi Nchini Kenya kwenye matibabu kufuatia kupigwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 akiwa mjini Dodoma na baadaye kusafirishwa na kwenda Kenya kwa matibabu.