Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameamuru eneo la Mererani Block A hadi D ujengwe ukuta wenye mlango mmoja na kamera zifungwe ili kuweza kukabiliana na wizi wa madini aina ya Tanzanite.

Ameyasema hayo hii leo Septemba 20, 2017 kwenye ziara ya kikazi mkoani Manyara katika Wilaya ya Simanjiro ambapo amesema ujenzi wa ukuta huo utasaidia kuondokna na wizi madini hayo hivyo serikali itaweza kukusanya mapato yake kikamilifu.

Aidha, Rais Magufuli amesema kuwa katika uongozi wake ameamua kuongoza vita ya kiuchumi, hivyo amewaomba Watanzania kushikamana pamoja ili kuweza kuishinda vita hiyo kubwa ya kiuchumi.

“Tanzanite ina eneo la kilometa za mraba 81.99, kuna block zimegawanywa. Tanzanite zinaibiwa sana, ni shamba la bibi, nafikiri mabibi waliokufa miaka mingi sana, sasa naviagiza vyombo vya usalama vianze kujenga ukuta kulizunguka eneo lote,”amesema Rais Dkt. Magufuli

Mbowe anena mazito kuhusu Lissu
Rodriguez aanza Bundesliga kwa kishindo