Umoja wa Vyama vya Demokrasia Afrika (DUA), umemchagua Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe kuwa Mwenyekiti mwenza wa DUA, katika mkutano mkutano mkuu wa umoja huo uliofanyika Novemba 9.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Chadema imeeleza kuwa Mbowe alichaguliwa katika mkutano mkuu wa vyama vya kidemokrasia uliofanyika Jijini Abidjan Ivory Coast ulioanza Novemba 9 mwaka huu.
Naye, Louisa Atta – Agyemang wa chama tawala cha Ghana, NPP naye amechaguliwa kuwa mwenyekiti mwenza atakayesaidiana na Mbowe ili kuleta mageuzi ya kimfumo na utendaji ndani ya DUA, kwa lengo la kukidhi mahitaji ya vyama.
Aidha, wenyeviti wenza wataongoza bodi ya watu nane itakayojumuisha makamu wenyeviti kutoka kanda tano za Afrika ambazo ni Morocco, Togo na Nigeria, Equatorial Guinea, Kenya na kusini Malawi.
Hata hivyo Mbowe atakuwa mmoja wa makamu wenyeviti wa Umoja wa Vyama vya Kidemokrasia Duniani (IDU), kutoka Afrika.