Rais wa Heshima na Mwekezaji Mwenza wa Klabu ya Simba Mohamed Dewji ‘Mo’ ameipongeza klabu ya Young Africans kwa kufanikiwa kutinga Hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Young Africans ilifanikiwa kushinda mtihani huo, kwa kuifunga Club Africain ya Tunisia 1-0, katika mchezo wa Hatua ya Mchujo Mkondo wa Pili uliopigwa jana Jumatano (Novemba 09) mjini Tunis, Tunisia.

‘Mo’ ametuamia kurasa zake za Mitandao ya kijamii kuwasilisha salamu zake za Pongeni kwa Young Africans, kwa kuitakia kila la kheri kwenye Hatua ya Makundi na kuikaribisha kwenye Ligi Kubwa.

‘Mo’ ameandika: Hongera sana Mtani, umeifaharisha Tanzania ! Katibu kwenye Ligi Kubwa ??#MpiraNiUmoja

Naye Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally ameipongeza Young Africans kwa mafanikio walioyapata kwa kuifunga Club Africain ya Tunisia, huku akiisisitiza klabu hiyo kupambana kwenye hatua ya Makundi.

Ahmed ameandika katika kurasa zake za Mitandao ya Kijamii: Jitihada tulizofanya kupeleka timu nne kwenye mashindanio ya kimataifa zimezaaa matunda.

Timu mbili kati ya nne tulizozipeleka CAF zitacheza makundi hongera Mtani?
Waliotuangusha ni Azam Fc na Geita Gold lakini nao wana muda wa kuendelea kujifunza.

Karibu Group Stage huku ndo sisi tunaishi.

Tunawakumbusha tuu mara yenu ya mwisho kushiriki makundi mliburuza mkia safari hii mna nafasi ya kufuta iyo aibu.

Well done ??

PICHA: Simba SC yerejea Dar es salaam, yaenda kambini
Mbowe Mwenyekiti mwenza Demokrasia Afrika