Jumla ya watu 14 wamefariki dunia, baada ya kutokea kwa shambulizi la ghafla katika msafara wa kijeshi wa waasi, wanaoungwa mkono naSerikali ya Iran katika eneo la mashariki mwa Syria lililo karibu na mpaka wa nchi ya Iraq.

Kwa mujibu wa Shirika la Syrian Observatory for Human Rights, linalofuatilia haki za binadamu nchini Syria, lenye makao yake nchini Uingereza limesema shambulizi hilo limefanywa katika malori yaliyokuwa yamebeba mafuta na silaha eneo la Albu Kamal.

Waokoaji wajaribu kuzima moto baada ya malori ya mafuta na mizigo kushambuliwa. Picha ya Twitter.

Kufuatia shambulio hilo, Muungano wa kijeshi unaoongozwa na vikosi vya kijeshi vya nchi ya Marekani umewaambia waandishi wa habari kwamba hauhusiki na shambulizi hilo.

Hata hivyo, Afisa mmoja wa ulinzi wa Irak amesema malori hayo yalikuwa yanasafirisha mafuta kutoka Iran kuelekea Lebanon, kupitia Irak na Syria ukijumuisha malori 22 ambapo 10 kati ya hayo yalishambuliwa baada ya kuingia Syria.

Uwanja wa Ndege wa Bukoba ni salama: TCAA
Mabadiliko hali ya hewa ni fusra: Bosi IMF