Mbunge wa viti maalum, Ester Bulaya ameishauri Serikali kutoa mafunzo ya kutumia silaha kwa vijana wachache wanaoshiriki mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) badala ya kuwafundisha wengi.

Amesema hayo leo Bungeni Jijini Dodoma wakati akimuuliza swali la nyongeza Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Elias Kwandikwa.

Bulaya amesema kuwa kutoa mafunzo ya silaha kwa vijana wengi wakati hawapati nafasi za kujiunga na jeshi hilo,  baadhi si waaminifu wanaweza kutumia mafunzo hayo kufanya uhalifu.

Aidha Waziri Kwandikwa  amejibu swali la nyongeza la Mbunge huyo, ambapo amesema jeshi hutoa mafunzo ya silaha kwa vijana katika idadi inayotakiwa na kwamba hakuna shida katika jambo hilo.

Wakati huohuo,   Serikali imetoa sababu za kuwarudisha nyumbani mapema vijana waliokuwa kwenye mafunzo ya JKT.

Kwandikwa ametaja sababu hizo ni kuangalia mtaala utakaosaidia kuboresha mafunzo na kuangalia muda wa mafunzo ya miezi mitatu ya waliomaliza kidato cha sita yafikie mwaka mmoja na kuwafanya vijana wapate ujuzi wa kujitegemea.

Waziri Kwandikwa ametoa majibu hayo kufuatia swali la msingi la Omari Issa Kombo aliyehoji sababu za kuwarejesha vijana ambao tayari walisharipoti kambini.

Shamimu na mumewe wahukumiwa kifungo cha maisha jela
Bumbuli: Kesho kikosi kitakua kamili