Mchungaji wa kanisa la New Life Prayer Centre, Ezekiel Odero, ambaye alikamatwa na Polisi akituhumiwa kwa mauaji ya watu 98 ambao ni waumini wa Kanisa la Good News International Ministry la Mchungaji Paul Mackenzie, ambaye pia amewahi kujinasibu kutibu ugonjwa wa Ukimwi – HIV, amefikishwa Mahakamani.
Odero amefikishwa Mahakamani hii leo, ambapo mara baada ya kusomewa mashitaka yanayomkabili atakuwa kizuizini hadi Mei 2, 2023 kesi hiyo itakapotajwa tena akihusishwa pia na vifo vingine vilivyotokea katika Kanisa lake baada ya kushawishi waumini wake kutorosha ndugu zao wagonjwa waliokuwa Hospitali na kuwapeleka kwake ili awaombee.
Mbele ya Mahakama ya shanzu iliyopo mjini Mombasa, Hakimu alitoa uamuzi huo baada ya Polisi kuomba muda zaidi ili kukamilisha uchunguzi juu ya tuhuma zinazomkabili Mchungaji huyo.
Mapema hivu karibuni ofisi ya DCI ilimhoji mmoja wa wachungaji wasaidizi wa Ezekiel ambaye alisema Mchungaji Mackenzie amekuwa akifadhiliwa
na Pastor Ezekiel na walikua ni washirika.
Mchungaji msaidizi huyo ambaye jina lake limehifadhiwa, alidai kuwa Mchungaji Mackenzie alikua akilazimisha watu kufunga
hadi kufa, na baada ya kifo Pastor Ezekiel alienda usiku wa manane kuchukua baadhi ya viungo vyao kabla ya kuzikwa.